Sisi ni
Iran Radio ni shirika la vyombo vya habari vya Iran ambalo lengo lake ni kutangaza na kuonesha taswira halisi na tofauti ya Iran sambamba na masuala mengine ya kimataifa. Mkusanyiko mkubwa wa matangazo ya sauti na media unafanya kazi ya kutangaza janibu kadhaa tofauti za Iran, kama vile masuala ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni ambayo mara nyingi huwa yanafumbiwa macho na vyombo vikuu vya habari au yanapotoshwa. Ni vivyo hivyo katika upande wa masuala ya kimataifa, Iran Radio inaakisi matukio hayo kwa namna tofauti sambamba na kutangaza mitazamo ya Iran kuhusu matukio hayo. Iran Radio inawalenga wale watu ambao wamechoshwa na utamaduni wa kila siku wa upashaji habari na wana kiu ya kupata kitu kipya cha kutegemewa.